25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Mwanafunzi achomwa kisu na kufariki akicheza kamari

Gurian Adolf -Nkasi

MWANAFUNZI wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Nkomolo wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Fredy Pupa (19) ameuawa kwa kuchomwa kisu wakati akicheza kamari, baada ya kudhulumiana fedha na mwenzake katika mchezo huo.

Kamanda wa Polisi Rukwa, Justine Masejo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa anaendelea na matibabu huku akiwa chini ya ulinzi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani uchunguzi utakapo kamilika.

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Mtanda, alisema tukio hilo lilitokea Januari 29 saa 11 jioni wakati mwanafunzi huyo akiwa na kijana aliyefahamika kwa jina la Samwel Nkoswe (20) wakicheza kamari.

Alisema mtuhumiwa wa mauaji hayo alikua ameacha shule na kuwa anaishi mtaani huku akijihusisha na vitendo haramu ikiwemo kucheza kamari, ambapo siku hiyo alikuwa akicheza na mwanafunzi huyo ambaye alikuwa ni rafiki yake.

Wakiwa wanacheza mchezo huo, ilinalezwa kuwa alikula fedha za mwanafunzi huyo, lakini alikataa kumpa pesa hizo, ndipo alipotoa kisu alichokuwa nacho mfukoni na kumchoma Fredy ubavuni karibu na tumboni kitendo kilichosababisha kuvuja damu nyingi na kupoteza maisha muda mfupi baadaye.

Baada ya kuona amefanya tukio hilo alikimbia na kwenda kujificha katika mashamba yaliyopo kijijini hapo, lakini wananchi walimsaka na kumkamata na kisha kumpa kipigo ambapo sasa yupo hospitali akipatiwa matibabu.

Alisema polisi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka kituo cha afya ambapo ulifanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu ambapo jana ulizikwa.

Wakati wa maziko hayo, mkuu huyo wa wilaya alitoa salamu za pole kwa familia iliyompoteza mtoto wao katika tukio hilo na kutumia nafasi hiyo kuwaonya wanafunzi kutojihusisha na mambo mengine tofauti na masomo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles