27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wataka wanafunzi wapimwe bikra kuepusha mimba, utoro

Gurian Adolf, Kalambo

BAADHI ya wazazi wilayani Kalambo mkoani Rukwa, wameiomba halmashauri hiyo kuanzisha mpango wa kuwapima bikira wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ili kuwabaini walioanza kujihusisha na vitendo vya ngono katika umri mdogo, hali itakayo changi kupunguza mimba na utotoni wilayani humo.

Ombi hilo walilitoa kwa nyakati tofauti wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, muda mfupi baada ya kikao kazi kilichowakutanisha Katibu Tawala wa wilaya hiyo,  Frank Sichalwe, na viongozi wa serikali za vijiji, kata na maofisa elimu kata waliopo katika maeneo ya mwambao wa ziwa Tanganyika.

Mmoja wa wazazi hao Getruda Siwale, mkazi wa Kijiji cha Kasanga, alisema imefika wakati Serikali kutumia njia hiyo kwani tatizo la mimba za utotoni na kwa wanafunzi limekuwa ni changamoto hivyo ni lazima zibuniwe mbinu zitakazo sababisha wanafunzi kuogopa kushiriki ngono.

Alisema nivema ukaanzishwa utaratibu wa kuwapima wanafunzi ujauzito na bikira kila baada ya miezi mitatu kwani hiyo itasaidia kwa kiasi kupunguza mimba za utotoni ambazo zimekua zikisababisha wengi kukatisha masomo.

Naye Peter Simuyemba, mkazi wa Kipanga wilayani Kalambo, alisema iwapo upimaji huo ukifanyika baadhi ya wanafunzi watakua waoga kujihusisha na mapenzi kwani watajua watabainika.

Alisema pia itawajengea heshima hata watakapo kuwa watu wazima na kuolewa kwani hata mila na desturi tangu zamani zilikua zikimpa thamani kubwa msichana anayeolewa na akiwa na bikira.

Mmoja wa wanafunzi anayesoma katika Shule ya Sekondari Matai, aliunga mkono ombi hilo, akisema iwapo mpango huo ukianza wanafunzi wengi wa kike wataacha kufanya ngono kwani wataingiwa na hofu kuwa iwapo wakibainika wamepoteza bikira itaonekana wameanza ngono hivyo watachukuliwa hatua.

Kwaupande wake katibu tawala wa wilaya hiyo, Sichalwe aliwaonya baadhi ya wazazi ambao hawatoi ushirikiano pindi watoto wao ambao ni wanafunzi wanapopata ujauzito.

Alisema kitendo hicho ni kinyume na sheria hivyo watambue kuwa huenda wakajikuta wanafikishwa mahakamani lengo likiwa ni kuhakikisha wilaya hiyo inafanikiwa katika kukabiliana na mimba kwa wanafunzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles