23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Mwamuzi fainali ASFC azua jambo Yanga

Na Winfrida Mtoi

Uongozi wa Klabu ya Yanga umesema umeshtushwa na chaguo la mwamuzi Ahmed Arajiga  kuwa ndiye atachezesha mechi yao ya fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC)dhidi ya Simba, utakaochezwa Jumapili, Julai 25, 2020 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Yanga leo, imesema samwamuzi huyo ndiye amehusika kuchezesha michezo ya wapinzani wao, zilizofuatana katika mashindano hayo ambayo ni robo fainali, nusu fainali na sasa fainali.

“Uongozi wa Yanga unaamini Tanzania ina waamuzi wengi wenye uwezo, hivyo kitendo cha kumrudisha mwamuzi mmoja katika mechi tatu za timu moja na shindano moja kinatia shaka kwetu kama klabu na mashabiki wetu pia,” imesema taarifa hiyo.

Wanajangwani hao wameomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na menejimenti ya mashindano hayo kujitafakari juu ya uamuzi wa kumtumia mwamuzi huyo katika mchezo wa mkubwa wa fainali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,303FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles