Azam FC inashusha vifaa tu

0
342

Klabu ya Azam imeendelea kufanya usajili baada ya leo kumsainisha mkataba wa miaka miwili kiungo mkabaji, Mzambia, Paul Katema kutoka Red Arrows ya  nchini humo.

Katema anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na Azam katika kuimarisha kikosi hicho kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu na michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Wachezaji wengine waliomwaga wino kwa Wanalambalamba hao ni  Wazambia, Charles Zulu, Rodgers Kola, Kenneth Muguna (Kenya) na Edward Manyama (Tanzania).

Kwa mujibu wa taarifa ya Azam, Katema ni  miongoni mwa viungo bora atakayeongeza nguvu katika kikosi hicho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here