30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

MWALIMU MBARONI KWA KILIMO CHA BANGI

Na AMON MTEGA – NYASA


WATU watano wakazi wa Wilaya ya Nyasa, Mkoa wa Ruvuma, akiwamo Mwalimu wa Shule ya Msingi Lipalamba, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani hapa kwa tuhuma za kujihusisha na kilimo cha bangi.

Taarifa hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Isabela Chilumba, alipokuwa akizungumuza na watendaji wa vijiji, kata pamoja na walimu wakati wa kikao cha wadau wa elimu wilayani hapa.

Alisema kwamba, watuhumiwa hao walikamatwa juzi baada ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo kufanya msako katika baadhi ya vijiji vinavyodaiwa kujihusisha na kilimo hicho.

“Pamoja na kwamba tunawashikilia watuhumuiwa hao, kwa sasa hatuwezi kuwataja kwa sababu bado tunaendelea kuwahoji ili tujue mtandao mpana wa wakulima wa zao hilo haramu,” alisema Chilumba.

Pamoja na hayo, mkuu huyo wa wilaya aliwataka maofisa watendaji wa kata na vijiji wilayani hapa, kuteketeza mashamba yote ya bangi kila wanapoyagundua.

Pia, alitaka wakulima wa zao hilo wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya dola ili sheria zichukue mkondo wake dhidi yao.

“Kuna baadhi ya watendaji wanawaogopa watu wanaojihusisha na kilimo hicho na jambo hili siwezi kulikubali kwa sababu unapokuwa kiongozi, hutakiwi kuogopa.

“Kwa hiyo, nawataka maofisa watendaji wa kata na vijiji, msiogope kuendesha mapambano dhidi ya watu wanaojihusisha na kilimo hicho kwa sababu Taifa limekuwa likiathiriwa na matumizi ya dawa hizo,” alisema.

Pamoja na hayo, mkuu huyo wa wilaya aliyataja mashamba yaliyoteketezwa hadi sasa, kwamba yako katika vijiji vya Mipotopoto na Lipalamba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles