24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MBUNGE ALILIA MAJI JIMBONI KWAKE

Na MWANDISHI WETU, PWANI


MBUNGE wa Rufiji, Mohamed Mchengerwa (CCM), ameiomba Serikali iwapelekee wananchi wa Kijiji cha Miangala Mpakani, huduma ya maji kwa kuwa wanatembea kilomita 12 kufuata huduma hiyo.

Mchengerwa alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa katika ziara jimboni humo ambapo alielezwa na wananchi, kwamba moja ya kero zinazowakabili ni uhaba wa maji.

"Wananchi wetu wapo nyuma katika maendeleo na huduma nyingi muhimu hakuna. Hili suala la maji ndilo tatizo kubwa, naiomba Serikali iwaangalie kwa jicho la pekee kwa kupunguza kero hiyo na changamoto nyingine kama za elimu, afya na barabara.

“Kero hiyo imesababishwa na jimbo letu  kusahaulika na kushindwa kutatuliwa kero walizonazo wananchi kwa kipindi kirefu.

“Pamoja na matatizo yanayowakabili wananchi hawa, bado wamekuwa wakijitolea katika kuleta maendeleo ya jimbo bila kulalamika.

"Kwa hiyo, nawashukuru wananchi wangu kwani mmeanza wenyewe jitihada za kujenga madarasa na naahidi kutoa mifuko 50 ya saruji pamoja na mabati ili kukarabati shule hii ambayo mmeipa jina la Mchengerwa,” alisema Mchengerwa.

Awali, Mshamu Muba ambaye ni mkazi wa kijiji hicho, alisema changamoto ya maji inawaumiza kwani wanaume wengi wanalea watoto ambao si wa kwao kutokana na wake zao kubakwa na kupewa mimba wakiwa wanatafuta maji umbali wa kilomita 12 kutoka majumbani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles