26.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

SONY MUSIC WAMSAINI WIZKID

LAGOS, Nigeria


STAA wa muziki nchini Nigeria, Ayodeji Balogun ‘WizKid’ amefanikiwa kusaini mkataba na kampuni ya Sony Music kwa ajili ya kusimamia kazi zake za muziki.

Dili hilo limekuja mara baada ya msanii huyo kufanya vizuri katika muziki nchini humo na duniani kote, hasa kutokana na kazi ambayo ameifanya na Drake, wimbo ambao unajulikana kwa jina la "One Dance".

Mkataba huo utamfanya msanii huyo kusimamiwa kazi za albamu zake duniani kote kama ilivyo kwa wasanii wengine ambao wamefanya kazi na kampuni hiyo ambao ni Chris Brown, John Legand, Tyga na wengine wengi.

“Ni ngumu sana kwa upande wangu kuamini kile ambacho ninakifanya, lakini ninaamini watu wanaona na ndiyo maana wananipa dili kubwa, nawashukuru sana Sony pamoja na RCA Records kwa kunipa dili la kusimamia kazi zangu, kikubwa ni kuzidi kukazana ili niweze kufika mbali zaidi,” alisema WizKid.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles