24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Mvua yavunja mchezo wa Man United na Man City

mou na guardiola

BEIJING, CHINA

MCHEZO wa kirafiki kati ya miamba wa Uingereza, Manchester City na Manchester United, ulifutwa jana kutokana na mvua kubwa ambayo ilinyesha juzi mjini Beijing nchini China.

Mchezo huo katika michuano ya ‘International Champions Cup’ (ICC), makocha wa timu hizo mbili, Pep Guardiola na Jose Mourinho, walikuwa wanatarajia kukutana kwa mara ya kwanza jana tangu wajiunge na klabu hizo za nchini England.

Mchezo huo ulitakiwa kupigwa kwenye uwanja wa Birds Nest, lakini ulishindikana kutokana na mvua hiyo ambayo ilinyesha kwa saa 11 na kuufanya mji huo kutawaliwa na maji hasa katika uwanja huo.

Hata hivyo, kocha wa Manchester City, Guardiola, mapema alihofia wachezaji wake kupata majeruhi kutokana na mvua hizo ambazo zinaendelea nchini humo.

Guardiola alidai kwamba kutokana na mvua hizo hali ya uwanja ni mbaya hivyo wachezaji wake wanaweza kupata majeruhi ambayo yanaweza kuwafanya wakawa na wakati mgumu katika msimu mpya wa ligi.

Hata hivyo, watabiri wa mambo ya hali ya hewa walisema kwamba mvua zaidi ingenyesha jana Jumatatu, lakini mvua hiyo ilianza mapema.

Waandaaji wa michuano hiyo walijaribu kutumia njia mbalimbali kwa ajili ya kuukausha uwanja huo lakini ilishindikana.

Inadaiwa kwamba tiketi 50,000 tayari zilikuwa zimeuzwa kwa ajili ya kuelekea kwenye mchezo huo.

Tayari Manchester United wamerejea jijini Manchester, wakati huo Manchester City wao leo hii wanaelekea mji wa Shenzhen kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Borussia Dortmund ya nchini Ujerumani, ambapo mchezo wao utapigwa kesho kutwa.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles