23.8 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Mhamiaji  kutoka Syria ajilipua Ujerumani

gettyimages-71967682-20160725012955-770x430

BONN: Ujerumani

MHAMIAJI kutoka Syria aliyekataliwa kupewa hifadhi  Ujerumani mwaka jana, amejilipua ndani ya baa  na kuwajeruhi wa 12, watatu kati yao wakiwa katika  hali mbaya.

Taarifa zinasema mtuhumiwa wa shambulio la kujitoa mhanga, anadhaniwa kuwa na uhusiano na mtandao wa ugaidi wa ISIS na alikuwa akisubiriwa kurudishwa Bulgaria.

Mtuhumiwa huyo ( 27), alijilipua katika mji wa Ansbach  saa 4.00 usiku katika tamasha la muziki lililokuwa na watazamaji zaidi ya 2,500 ambao waliondolewa na kusimamishwa tamasha hilo ili kuimarisha ulinzi.

Hilo ni shambulio la tatu  Bavaria  katika kipindi cha wiki moja.

Ijumaa iliyopita, watu tisa waliuawa katika shambulio la ufyatuaji risasi mjini Munich lililofanywa na kijana Ali Sonboly (18).

Kabla ya hapo, kijana mwingine aliwashambulia watu kwa kisu na shoka katika  treni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,718FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles