22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

 Clinton aishitumu Urusi kufanya udukuzi

 Hillary Clinton
Hillary Clinton

WASHINGTON: Marekani

VIONGOZI wa ngazi za juu wa kampeni za Mgombea wa urais wa Marekani wa Chama cha Democrat, Hillary Clinton wameishutumu   Urusi kwa kuwa mstari wa  mbele kukichafua chama hicho    kumsaidia mpinzani wake,Donald Trump  wa Chama cha Republican.

Maofisa wa usalama wa Marekani wamekuwa  na wasiwasi na kuituhumu  Urusi kwa kuingilia masuala ya uchaguzi ya nchi hiyo.

Wiki iliyopita, saa chache kabla mtandao wa WikiLeaks kutoa taarifa za siri za chama cha Democrat, Ikulu ya Marekani iliitisha mkutano wa maofisa wa ngazi za juu wa usalama kujadili ripoti ya Urusi kuwa ilikuwa imefanya udukuzi wa mtandao wa Kamati ya chama cha National Democrat.

Hata hivyo, wataalamu wengine bado wana wasiwasi na Urusi katika madai hayo ambayo yamesababisha mshituko ndani ya kampeni ya Clinton na pia usalama wa taifa la Marekani.

Maofisa kutoka taasisi za ujasusi na ulinzi likiwamo baraza la usalama wa taifa, idara ya ulinzi, FBI na idara ya usalama wa ndani, waliudhuluria mkutano huo usiku kabla kutolewa  barau pepe za siri kwenye matandao wa WikiLeaks.

Wachambuzi wanasema  kama mashitaka hayo ni ya kweli, itakuwa ni mara kwanza Urusi kujaribu kuingilia uchaguzi wa Marekani kwa njia hiyo.

Gazeti la Washighton Post limeandika kuwa Kiongozi mkuu wa kampeni ya Clinton, Robby Mook, aliliambia Shirika la Habari la ABC Jumapili iliyopita kuwa wameambiwa na wataalamu kuwa watendaji wakuu kutoka Urusi walifanya udukuzi kwenye chama cha Democrat na kuchukua barua pepe ambazo hivi sasa wanazivujisha katika mitandao.

“Wataalamu wanatuambia kuwa Urusi ndiyo inahusika kwa lengo la kumsadia Donald Trump,” wamesema maofisa hao.

Maofisa wa kampeni ya Trump wamepinga mashitaka hayo na kudai kuwa ni mawazo ya upuuzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles