26.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Mv Liemba: Meli kongwe ya Kijerumani iliyobeba historia

M.V. Liemba
M.V. Liemba

NA FARAJA MASINDE,

NI karne nzima tangu kuwapo kwa Meli ya Kijerumani Graf von Götzen, maarufu kwa jina la MV Liemba. Inapatikana mkoani Kigoma Magharibi mwa Tanzania.

Meli hii ambayo hufanya safari zake Ziwa Tanganyika licha ya kubeba abiria na mizigo yao, pia imebeba historia na kivutio kikubwa cha utamaduni.

Kigoma ni Mkoa wa Magharibi ya Tanzania ulio kwenye ufukwe wa upande wa Mashariki wa Ziwa Tanganyika.

Meli ya MV Liemba, inayomilikiwa na Shirika la Reli la Tanzania, hufanya safari za kuelekea Mpulungu, Zambia na Kassanga, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Hakuna anayeweza kusema hasa, ni safari ya ngapi meli hii ya Liemba imeng’oa nanga na kutoweka katika bandari ya Kigoma.

Hii ni miongoni mwa meli chache duniani kuishi na kuendelea kufanya kazi kwa karibu karne nzima sasa.

Mwaka jana, meli hii ya Liemba ilitimiza miaka 100, karne tangu ianze kuelea kwenye Ziwa Tanganyika, ambapo ililetwa na Wajerumani mwaka 1915.

Mwaka 2007 ilichapishwa katika jarida la GEO la nchini Ujerumani na hivyo kuongeza thamani kubwa ya meli hiyo ambayo kwa sasa inasimamiwa na Marine Service Company Ltd kama waendelezaji wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles