27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

Historia ya mafuta, gesi Tanzania

picha+saba

NA FARAJA MASINDE,

WIKI iliyopita tuliishia awamu ya pili ambayo ilikuwa ni kuanzia mwaka 1969-1979. Leo tunaendelea na historia hii.

Baada ya kuanzishwa kwa TPDC, mkataba wa kwanza wa kuchangia uzalishaji (PSA) ulisainiwa kati ya TPDC na AGIP (Aziende Generale Italian Petroli – kampuni ya mafuta ya Italia) kwenye eneo ambalo lilikuwa chini ya usimamizi wa kampuni za BP na Shell katika wa awamu ya kwanza.

Historia inaendelea kutueleza kuwa mwaka 1973, AGIP aliingia ubia na kampuni ya AMOCO na kuchimba visima vitano, vitatu ufukweni na viwili mbali na ufukwe.

Taarifa nyingine zinaonyesha kuwa jumla ya visima sita vilichimbwa na AGIP na AMOCO huku vitatu vikiwa ufukweni na vitatu mbali na ufukwe, uchimbaji huu ulisababisha ugunduzi mkubwa kule Songo Songo mwaka 1974.

Ugunduzi huo ulithibitishwa na TPDC katika programu yake ya visima vitatu iliyotekelezwa kuanzia mwaka 1975 hadi 1979. Kuanzia 1978, TPDC ikaingia katika utafiti kwenye maeneo ya ufukweni na mbali na ufukwe. Utafiti wa ufukweni ulijumuisha maeneo ya Ruvu, Kimbiji/Bigwa, Pemba, Mafia na Ruvuma, wakati ule wa mbali na ufukwe ulijumuisha Songo Songo, Pemba na Zanzibar.

Awamu ya Tatu: 1980-1991

Ni katika kipindi hiki ambapo Serikali ilitunga Sheria ya Petroli (Utafiti na Uzalishaji) Tanzania mwaka 1980, na kugundulika kwa gesi katika eneo la Mnazi Bay. Kati ya awamu hizi tano, uchimbaji mwingi ulitokea katika awamu hii ya tatu na hii ilisababishwa na kutungwa kwa sheria ya petrol na kupanda kwa bei ya petrol mwanzoni mwa miaka ya 1980.

TPDC iliingia katika uendelezaji wa Songo Songo kwa kuchimba visima viwili vya Kimbiji Mashariki-1 na Kimbiji Kuu-1. Kampuni za Sheli, IEDC (Shirika la Kimatatifa la Maendeleo ya Uchumi) na Camarco group, Elf na AMOCO walipewa leseni za utafiti wa mafuta na gesi. Kampuni ya Shell na baadaye Esso walipewa leseni tano zinazochukua maeneo ya Ruvu na Bonde la Selous mwaka 1981.

Awamu ya nne: 1992-1999

Awamu hii ilikuwa na shughuli chache za utafiti katika miaka yake ya mwanzo, kulikosekana waombaji wapya wa kufanya tafiti na uamuzi wa serikali kuendeleza zaidi maeneo ya uchimbaji eneo la Songo Songo yaligubika shughuli nyingine.

Kampuni ya serikali, TPDC na Shirila la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), wakishirikiana na kampuni za Canada, Ocelot na Trans-Canada pipelines, walijishughulisha na uendelezaji, usambazaji na utumiaji wa nishati katika eneo la Songo Songo.

Kutolewa kwa leseni za utafiti mwaka 1995 katika mabonde ya pwani kwa kampuni ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Tanganyika Oil Company, Exon Mobil, Shell, KUFPEK (Kampuni ya Kigeni ya Utafiti wa Petroli ya Kuwait) na AMOCO kuliongeza kasi ya shughuli za utafiti.

Tanganyika Oil Company ilichimba visima viwili katika Bonde la Mandawa mwaka 1996/97. Pia, makubaliano ya utafiti yalitiwa saini kati ya TPDF na kampuni ya Canada ya Antrim Resources (sasa hivi inaitwa Atrim Energy Limited) na Canop World-Wide na Ndovu Resources ya Australia.

Usikose wiki ijayo, kwa maoni 0653045474.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles