25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Museveni, Kagame wasaini kubadilishana wafungwa

LUANDA, ANGOLA 

RAIS wa Rwanda Paul Kagame na Rais wa Uganda Yoweri Museveni wamesaini makubaliano ya kubadilishana wafungwa, baada ya mazungumzo ya upatanishi yaliyoongozwa na Angola mjini Luanda juzi. 

Hakukuwa na taarifa zaidi kuhusu idadi ya wafungwa watakaoachiwa, wala muda wa kuachiwa kwao baada ya tukio hilo adhimu. 

Marais hao, Kagame na Museveni waliwahi kuwa washirika wakubwa, lakini urafiki wao umegeuka uhasama, huku kila nchi ikiituhumu nyingine kuendesha ujasusi dhidi yake, na kuyasaidia makundi ya waasi yanayonuiya kuiangusha serikali yake. 

Katika mkutano wa juzi ambao ulimshirikisha pia rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi, Kagame na Museveni walikubaliana kukutana tena Februari  21  mwaka huu, kwenye mpaka wa Gatuna kati ya nchi zao. 

Mwezi Agosti mwaka jana nchi hizo zilisaini makubaliano ya kuboresha uhusiano wa kisiasa na wa kibiashara, lakini hakukuwa na maendeleo ya maana hali inayoonyesha kuwa kila mmoja alikuwa na hofu na mwenzake.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles