Ciara atarajia mtoto wa tatu

0
512

New York, Marekani

NYOTA wa muziki nchini Marekani Ciara Harris, aliwahi kusema lengo lake ni kuwa na familia kubwa, hivyo mrembo huyo anatarajia mtoto wa tatu na mume wake Russell Wilson.

Mastaa hao wametumia kurasa zao za mitandao ya kijamii na kuweka wazi kuwa wanatarajia kuongeza mtoto siku za hivi karibuni.

Mtoto huyo atakuwa wa tatu kwa Ciara, lakini atakuwa wa pili kwa Wilson. Awali Ciara alipata mtoto wa kwanza wakati yupo kwenye uhusiano na rapa Future na kisha kupata mtoto anayejulikana kwa jina la Future Zahir mwenye miaka mitano mitano.

Ciara aliposti picha kwenye Instagram yake akionesha tumbo na kisha kuandika ‘Namba 3’ wakati huo Wilson akiposti picha akiwa na mrembo huyo na yeye kuandika namba 3, wakimaanisha wanatarajia mtoto mwingine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here