– N’Djamena
Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Chad, Luteni Mahamat Idris Deby maarufu kama ‘General Kaka’ mwenye umri wa miaka 37 ateuliwa kuongoza Taifa la Chad kwa kipindi cha mpito cha mwaka mmoja kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu.
Uteuzi huo uliofanywa na Baraza la Mpito la wanajeshi la wanachama 15 (TMC) linaundwa na majenerali ambao wataiongoza Chad kwa muda wa miezi 18.
Rais Deby, ambaye aliongoza Chad kwa miongo mitatu, alifariki saa kadhaa baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais kwa kura asilimia 80% aprili 11, 2021.
Katika taarifa iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii jana usiku, FACT ilisema: “Vikosi vya upinzaji viko katika milango ya mji wa N’Djamena
Pia waasi kutoka chama cha Front for Change and Concord in Chad (FACT) wameripotiwa kuanza tena harakati zao kuelekea mji wa N’Djamena, baada ya kifo cha Deby.