-Kinshasa
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amewasili mjini Kinshasa katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa ziara ya siku tatu kwa mwaliko wa Rais Felix Tshisekedi.
Rais, Uhuru amepokelewa na Rais Tshisekedi, Maafisa wa serikali ya Kongo, Waziri wa Mambo ya Nje, Christopher Lutundula Pamoja na Gavana wa Jiji la Kinshasa, Gentiny Ngobila Mbala.
Rais Kenyatta na mwenyeji wake Rais Tshisekedi leo watafanya mazungumzo ya ushirikiano baina ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na kusaini makubaliano mbali mbali ya ushirikiano baina ya nchi hizo.