31.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 5, 2022

Contact us: [email protected]

Mtoto wa Mbunge mbaroni kwa ujangili

Mgombea ubunge Jimbo la Mbarali haroon-mulla
Mgombea ubunge Jimbo la Mbarali haroon-mulla

Na Pendo Fundisha-Mbeya

MTOTO wa Mbunge wa Mbarali, Haroon Mulla (CCM), ametiwa nguvuni kwa tuhuma za kukutwa na meno ya tembo pamoja na nyama ya pori kinyume cha sheria.

Tukio hilo lilitokea jana wilayani Mbarali ambapo mtoto wa mbunge huyo alikamatwa na shehena ya meno ya tembo pamoja na nyama hiyo ambayo haijajulikana kiasi chake.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya vyombo vya dola mkoani hapa, kilimbia MTANZANIA  kuwa baada ya tukio hilo maofisa wa Serikali pamoja na askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) walimtia mbaroni mtu huyo ambapo hadi tunakwenda mitamboni walikuwa wakiendelea na mahojiano kwa lengo la kubaini mtandao wa ujangili anaoshirikiana nao.

“Ukitaka kufahamu nani mmiliki halali wa biashara hiyo baba au mtoto, tungependa Serikali ifuatilie silaha alizokutwa nazo mtuhumiwa, kwani hapo ndiyo ukweli utajulikana, Serikali imekuwa  ikiingia hasara kutokana na kuuawa kwa tembo, hivyo ni vema suala hili likachunguzwa kwa kina,” alisema mtoa habari wetu.

Chanzo hicho kilisema kuwa familia hiyo imekuwa ikihusishwa na tuhuma za ujangili pamoja na kufanya biashara ya meno ya tembo kwa miaka mingi.

Kutokana na taarifa hiyo MTANZANIA lilimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari, ambaye alikiri kukamatwa kwa watu hao, huku akisema walikamatwa na askari wa Tanapa.

“Mtuhumiwa bado yupo kwenye mikono ya Tanapa hivyo kwa sasa siwezi kuzungumzia suala hili. Kwani operesheni hii inaendeshwa na Tanapa wenyewe.

“…na huyo mtu yupo mikononi mwao mimi siwezi kulizungumzia ila watakapomfikisha kwetu, ndiyo nitatolea taarifa kwa sasa sina uwezo nalo,” alisema Kamanda Kidavashari.

Kutokana na hali hiyo MTANZANI ilipomtafuta Meneja Mawasiliano wa Tanapa, Pascal Shelutete ili kupata ufafanuzi wa tukio hilo akiri kukamatwa kwa mtoto huyo wa mbunge na kueleza kuwa wanaendelea na uchunguzi.

“Ni kweli tunamshikilia mtuhumiwa na tunaendelea naye na uchunguzi na ukikamilika tutatoa taarifa kwa umma,” alisema.

MTANZANIA lilipomtafuta mbunge huyo ili kuzungumzia taarifa za mtoto wake kuhusishwa na mtandao wa ujangili, hakuweza kupatikana kutokanana simu yake ya mkononi kuita bila kupokewa.

“Mheshimiwa salaam, kuna taarifa za mtoto wako kukamatwa kwa tuhuma za ujangili wilayani Mbarali, je ni kweli?,” ulieleza ujumbe huo ambao hakuujibu hadi tunakwenda mitamboni. Hata hivyo hivyo jitihada za kumpata mbunge huyo zinaendelea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,586FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles