28.3 C
Dar es Salaam
Saturday, November 26, 2022

Contact us: [email protected]

Kikwete asimulia changamoto za UDSM

jakaya-kikwetePATRICIA KIMELEMETA NA JOHANES RESPICIUS -Dar es Salaam

MKUU wa Chuo Kikuu cha Dar es Saalam (UDSM) na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, amesimulia alichokikuta chuoni hapo baada ya kuteuliwa kuwa mkuu wake, Januari 17 mwaka huu.

Kikwete aliteuliwa na rais Dk. John Magufuli kushika wadhifa huo baada ya aliyekuwa mkuu wa chuo hicho, Balozi, Fulgence Kazaura, kufariki dunia Februari 2014.

Akizungumza katika kongamano la miaka 55 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho, Kikwete alisema baada ya kuteuliwa alikutana na wakurugenzi wa chuo hicho na kujadili changamoto mbalimbali zinazokikabili ikiwamo mikopo, hosteli, maktaba na miundombinu mibovu ya chuo hicho kwa sababu ni kikongwe kuliko  vyuo vingine nchini.

Kutokana na hali hiyo aliwasiliana na Rais Dk. Magufuli na kumweleza changamoto hizo ili kuangalia namna ya kuzitatua ikiwamo kuanza ujenzi wa mabweni ambayo yana uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 4000.

 

MIKOPO

Akizungumzia mikopo, Kikwete alisema licha ya kuwapo kwa matatizo ya mikopo kwa baadhi ya wanafunzi, atashirikiana na wadau mbalimbali ikiwamo Serikali na wazazi ili kuhakikisha wanafunzi wenye mahitaji ya mikopo wanapewa kipaumbele.

“Katika kipindi changu cha ukuu wa chuo, nitahakikisha naunganisha uongozi wa chuo na wadau mbalimbali ikiwamo serikali ili kuhakikisha wanafunzi wasio na uwezo wanapata mikopo,”alisema.

Kutokana na hali hiyo, atahakikisha kuwa chuo hicho kinakua bora kuliko vyuo vyote nchini ili kiweze kuendana na umri wake tangu kilipoanzishwa ikiwamo utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi ili waweze kupata viongozi wazuri.

Akizungumzia mafanikio ambayo chuo hicho kimeyapata, Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Rwekaza Mukandala alisema chuo hicho kwa sasa kinaweza kupokea wanafunzi zaidi ya 80,000 kutoka ndani na nje ya nchi.

“Kwa sasa tunazungumzia UDSM kupokea idadi kubwa ya Watanzania  na watu wa mataifa mengine zaidi ya 80,000 kuja kujifunza.

“Hata hivyo chuo kimekuwa kikishirikiana kikamilifu katika kuboresha ustawi wa binadamu katika aina mbalimbali ya nafasi na majukumu kama vile marais, makamu wa Rais, viongozi wa vyama vya siasa, mawaziri wa serikali, majaji wakuu, wanasheria na watendaji wakuu.

“Chuo  kikuu kimetoa wasomi na watafiti ambao wametoa michango mikubwa katika kujenga miamko ya kimaendeleo  hususani katika maeneo ya mabadiliko ya tabia nchi, sheria ya bahari, maendeleo endelevu, utawala, tafiti za majini na haki za binadamu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,558FollowersFollow
557,000SubscribersSubscribe

Latest Articles