23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

MTOTO WA LOWASSA AMSHANGAA MWANAMKE ANAYEDAI NDUGU YAO

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mtoto mkubwa wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Fred Lowassa, ameshangaa mwanamke aliyejitokeza na kudai kuwa ni binti wa mwanasiasa huyo.

Aidha, amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutumia vizuri mamlaka yake.

Kauli hiyo ya Fred imekuja saa chache baada ya mwanamke mmoja mkazi wa Kigamboni, Fatuma Lowassa (31), kujitokeza katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, leo Jumanne Aprili 10, akidai kutelekezwa na baba yake ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.

Akiwa Monduli mkoani Arusha, Fred ametoa tamko akisema; “Nimesikia mwanamama mmoja akiongea kuwa yeye ni ndugu yetu kule Dar es Salaam.

“Kwa taarifa tu sisi watu wa Monduli kwetu watoto ni baraka na neema, nimeshangaa ametukosa ukoo mzima kujitambulisha.

“Namwambia Paul Makonda, nimetoka naye mbali sana, nasikitika sana anavyotumia nafasi yake vibaya kwa manufaa anayoyajua. Makonda nimekulea.” Ameandika Fred.

Mwanamke huyo amejitokeza leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ikiwa ni mwendelezo wa Makonda kuonana na wanawake waliotelekezwa na watoto na waume zao.

Mwanamke huyo amesema yuko tayari kupima kipimo cha DNA na Lowasa kuthibitisha kama kweli ni baba yake huku akijinasibu kumtafuta baba yake huyo kwa muda mrefu bila mafanikio.

“Nilipeleka barua Ikulu kuomba kuonana na baba kipindi akiwa Waziri Mkuu lakini niliitwa mimi na mama katika Klabu ya Mamba iliyopo Kinondoni, alikuja mwanamume akiwa kwenye gari lenye ‘tinted’ akatuhoji mimi na mama akaondoka hakutupa majibu yoyote hadi leo,” amesema Fatuma.

Aidha, amesema aliwahi kukutana na Fred na akamuahidi kumsaidia lakini hadi sasa amekuwa kimya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,244FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles