29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

MSIBA WA PATRICK UTATA MTUPU

NA MWANDISHI WETU


 

MSIBA wa mtoto wa msanii, Rose Nungu maarufu kwa jina la Muna Love, aliyejulikana kwa jina la Patrick Peter, umeingia kwenye utata baada ya familia kuingia kwenye mzozo.

Mzozo huo umekuja baada ya mama mzazi kutaka msiba huo ukae nyumbani kwake Mbezi Jogoo jijini Dar es Salaam, huku familia pamoja na baba wa mtoto huyo ukihitaji msiba huo uwepo Mwananyamala jijini.

Patrick aliyepata umaarufu katika mitandao ya kijamii kwa kutangaza maduka ya nguo za watoto, alipoteza maisha juzi nchini Kenya alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na tatizo la uvimbe kichwani.

Mama mzazi wa Muna alisema wameamua kuweka msiba Mwananyamala kwa sababu ndiko nyumbani kwa baba yake.

“Msiba hauko Mbezi, Patrick alikuwa na baba yake na yupo hai anaitwa Peter Kosovo, hivyo msiba upo Mwananyamala na mipango ya kurudisha mwili Tanzania kwa ajili ya maziko inaendelea,” alisema.

Mama huyo aliomba watu waachane na habari zinazosambazwa kwenye mitandao kuwa mtoto huyo ni wa mtangazaji maarufu wa televisheni, Castro Dickson.

Peter Kosovo ambaye ni baba mzazi wa Patrick, amesema amepokea kwa uchungu kifo cha mtoto wake wa pekee.

“Nilipata taarifa kutoka kwa mke wangu, nilimtumia pesa za matibabu pia mtoto nilimkatia bima kubwa ambayo ndiyo aliyokuwa akitibiwa nayo Hospitali ya Muhimbili hapo awali,” alisema Kosovo.

Aliongeza kuwa hakutaka mtoto wake akatibiwe Kenya kwa sababu ana daktari wake na hakushindwa kumtibia ila mama alikataa akampatia fedha ya usafiri.

“Nilitoa milioni 2 ya tiketi ya ndege ya kwenda Nairobi, ila nimekuja kusikia walienda na gari kitu ambacho kiliniumiza,” alisema Peter.

Miongoni mwa watu waliojitokeza kwenye msiba Mwananyamala ni Wema Sepetu na mama yake, wakati huo marafiki wa Muna walikusanyika nyumbani kwake Mbezi Jogoo, huko nako baadhi ya watu waliokusanyika ni pamoja na Husna Sajent na Zamaradi Mketema.

Hata hivyo, Muna amedai mwili wa marehemu utawasili Ijumaa huku upande wa baba wa mtoto wakibakiwa na sintofahamu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,335FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles