YULE msanii wa maigizo chipukizi aliyeshinda milioni 50 katika shindano la Tanzania Movie Talent (TMT), Denis Lwasai, anatarajiwa kuwasili jijini Arusha leo akitokea jijini Dar es Salaam ambako shindano hilo lilifanyika.
Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gazeti hili, mshindi huyo anatarajiwa kuanzia msafara wake kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa KIA asubuhi ambapo watu mbalimbali wameombwa kufika kwa ajili ya kumpongeza mshindi huyo pamoja na kupiga naye picha za kumbukumbu.
Mshindi huyo aliyewahi kufanyakazi na marehemu Steven Kanumba, aliibuka na kitita hicho na kuwashinda wenzake 10 walioingia katika fainali.