28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Ne-Yo, Kiba warekodi pamoja

ali-kibaMSANII maarufu wa R&B kutoka nchini Marekani, Ne-Yo, amerekodi wimbo na baadhi ya wasanii wa Afrika akiwemo msanii Ali Kiba kutoka Tanzania, katika onyesho la Coke Studio msimu wa tatu lililofanyika hivi karibuni, Nairobi, Kenya.

Wasanii wengine walioshirikiana na Ne-Yo ni Maurice Kirya (Uganda), Wangechi (Kenya), Dama Do Bling (Msumbiji) na Ice Prince (Nigeria).

“Nimefurahi sana kuona watu wakinisapoti, muhimu ni kujituma katika kile tunachofanya ili tutimize malengo yenu kwa sababu juhudi ndio kila kitu,” alisema Ali Kiba.

Kwa upande wake Ne-Yo alisema ni heshima kubwa kupata fursa ya kufanya kazi na wasanii wenye vipaji vikubwa kutoka barani Afrika na hilo linasaidia sana kuunganisha watu bila kujali makabila yao, rangi wala dini zao.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles