Kabla ya arobaini, Bobby Brown afanya shoo

0
744

150214-news-bobby-brownNA BADI MCHOMOLO

NYOTA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Bobby Brown, juzi alipanda jukwaani na kufanya onyesho la kwanza tangu kifo cha mtoto wake, Kristina kilichotokea Julai mwaka huu.

Kristina alizikwa Agosti 3 mwaka huu, hivyo siku 23 tu zimepita amefanya onyesho huku akiwashukuru waliohudhuria onyesho hilo.

“Nawashukuru sana kwa uwepo wenu siku ya leo, pia nawashukuru wale wote mliomuombea mwanangu wakati alipokuwa akiugua,” alieleza Brown.

Hata hivyo, wakati baba huyo akitumbuiza, aliyekuwa mpenzi wa binti yake huyo aliyefariki, Nick Gordon, alitembelea kaburi la mpenzi wake huyo kwa mara ya kwanza baada ya kuzuiwa kuzika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here