30.8 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

MSAKO POMBE ZA VIROBA KUANZA KESHO

Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM


SERIKALI imetangaza kuanza msako wa kukamata pombe kali aina ya viroba katika maeneo mbalimbali nchini kuanzia kesho.

Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa atakayekutwa ameingiza nchini, kusambaza na kutumia aina ya kilevi hicho.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba,  alisema kuanzia kesho utekelezaji wa kupiga marufuku pombe hizo utaanza na utakakwenda sambamba na msako mkali.

Alisema kwa atakayekutwa ameingiza nchini pombe hizo atatozwa faini ya Sh milioni 5 na kifungo cha miaka 2, wakati atakayezalisha atatozwa faini ya Sh milioni 2 au kifungo cha miaka 2.

Alisema atakayeuza au kusambaza faini Sh 100,000 na kifungo cha miaka 2 na atakayekutwa anatumia atalipa faini ya Sh 50, 000 na kifungo cha miaka 3.

Waziri January, alisema ni muhimu wawekezaji, wafanyabiashara na watumiaji kufuata sheria ya vileo inayoelekeza mahali pa kuuza pombe  na muda wa kutumia na sio kuuzwa kwa wauza vocha.

Alisema malighafi pia zinazotengeneza pombe hizo,kampuni na taasisi zinazoingiza  zitasajiliwa ofisi ya Mkemia Mkuu  na kutolewa leseni.

January alisema katika kazi hiyo msajili atawajibika kutoa taarifa sahihi za majina ya makampuni na watu binafsi na taasisi zinazohusika kiasi kilichoingizwa na kimetumika pamoja na madhumuni ya matumizi.

“Vifungashio vinavyohitajika ni mil. 200 na wenye mitambo ya kuzalisha pombe hizo wajue hatima yao kwa kuwa ikibainika inatumika itataifishwa na kuchukuliwa hatua.

“Nimepokea malalamiko kuhusu hatua hiyo ya serikali na tumezingatia sheria na suala la muda umezingatiwa kwa kuwa tangazo hilo lilitolewa mapema bungeni,” alisema January.

Alisema suala la kuwapa muda wafanyabiashara hao utatolewa kwa wazalishaji wenye ushahidi wa kuhama katika vifungashio.

Hata hivyo alisema ameziagiza mamlaka mbalimbali kuanza utekelezaji wa kazi hiyo mara moja ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (T R A) kusimamia mfumo wa stempu za kielektroniki ili kudhibiti ujazo wakati wa uzalishaji kwa ajili ya kupata mapato stahiki.

Waziri huyo pia ameitaka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Watoto na Wazee, kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)  pamoja na mabwana afya katika opersheni hiyo kutoa elimu kwa umma na kukagua maeneo yote yanayotumika kuhifadhia kuuza na kusambaza vileo vya aiba zote na kushiriki kukamata vileo ambavyo vipo kinyume cha sheria na kanuni

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles