25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mrema ataka marekebisho sheria Bodi ya Parole

FLORENCE SANAWA – Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Bodi ya Parole anayemaliza muda wake, Augustine Mrema, amesema maboresho ya Sheria ya Bodi ya Parole yanapaswa kufanyika ili wafungwa wa vifungo virefu na maisha waweze kunufaika.

Hayo aliyasema jana wakati akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Salasala.

Alisema wafungwa wa vifungo virefu, wamekuwa hawanufaiki na mpango huo hali iliyosababisha bodi hiyo kutoa mapendekezo hayo.

Alisema bodi zilizopita zimekuwa zikitoa mapendekezo ya wafungwa wenye vifungo virefu na wale wa maisha ambao ndio walengwa wa mpango huo.

Katika hatua nyingine, Mrema alisema kasi ya utendaji kazi wa bodi hiyo imekuwa ndogo, ikishindwa kukidhi mahitaji kutokana na fedha kutengwa kiasi kidogo.

Ufinyu huo wa bajeti umesababisha idadi ndogo ya majalada yanayowasilishwa na bodi za mikoa ukilinganisha na idadi ya wafungwa wenye sifa walioko magerezani.

 “Unajua mwaka 2004 zilinunuliwa pikipiki 25 ambazo zilitumiwa na bodi hiyo, hivi sasa ni mbovu, hivyo wajumbe wa bodi hiyo kutembea umbali mrefu kufuatilia taarifa za wafungwa walioachiwa kwa parole kutokana na kukosa usafiri.

“Wakati mwingine hizi mahakama za mwanzo na wilaya zimekuwa zikikwamisha kutoa hukumu za wafungwa, hivyo kuwafanya kukaa gerezani kwa muda mrefu zaidi,” alisema Mrema.

Alisema bodi yao imefanya kazi nzuri hata ukiangalia kati ya wafungwa 648 walioachiliwa kwa mpango wa parole, hakuna aliyevunja sheria na kurudishwa gerezani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles