24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunge wanawake waliobaguliwa na Trump wajibu mapigo

WASHINGTON DC, MAREKANI

WABUNGE wanne walioshambuliwa na Rais Donald Trump, katika mfululizo wa maandishi ya tweeter yanayodaiwa kuwa ya ubaguzi, wamepuuza maneno yake wakisema ni kujaribu kuwaondoa katika umakini wao.

Wawakilishi hao, Alexandria Ocasio-Cortez, Ilhan Omar, Ayanna Pressley na Rashida Tlaib, wakizungumza na waandishi wa habari wamewataka wananchi wa Marekani kutoyatilia maanani maneno ya Trump.

Trump alisema wanawake hao wanne waondoke Marekani huku akitetea kauli zake na kukataa shutuma kuwa ni mbaguzi.

Wanawake hao walisema hivi sasa watu waweke akili zao kwenye sera za Marekani na si maneno ya Trump.

Kwa pamoja Ilhan na Rashida wamerejea wito wa kutaka Trump apigiwe kura ya kutokuwa na imani naye.

“Kikosi chetu ni kikubwa. Kikosi chetu kinahusisha mtu yeyote aliye tayari kujenga ulimwengu wa usawa na haki,” alisema Ayanna.

Ilhan alisema maneno ya Trump yanadhihirisha mashambulizi ya ubaguzi wa rangi dhidi ya wanawake wanne maneno ambayo hayana maana yeyote isipokuwa kuigawanya nchi.

Awali Trump alisema kuwa Ilhan alikuwa akiunga mkono kundi la wanamgambo wa al-Qaeda.

“Ninajua kila Muislamu aliyeishi nchini humu na duniani kote amesikia kuhusu kauli hiyo, hivyo sitaipa nafasi kwa kuijibu,” alisema Ilhan.

Aliongeza kuwa hakutegemea jumuia ya watu weupe kujibu baada ya mtu mweupe ‘kuua kwenye shule au jumba la sinema, msikiti au sinagogi’.

Alexandria alisimulia kuhusu alipotembelea Washington DC akiwa mtoto, akisema watu wawaambie watoto wao kuwa ‘chochote kile atakachosema Rais, nchi hii ni yenu’.

Wanawake wote wanne wamesisitiza kuwa huduma za afya, matumizi mabaya ya silaha, kushikiliwa kwa wahamiaji katika mpaka kati ya Marekani na Mexico ni masuala ya kutazamwa.

Spika wa Bunge, Nancy Pelosi, alinukuu ujumbe wa Trump na kutaja maneno yake ya kibaguzi.

“Wakati Donald Trump anawaambia wabunge wanne wa Marekani warudi nchini mwao, anathibitisha mpango wake wa ‘Make America Great Again’ unahusu kuifanya Marekani liwe taifa la watu weupe kwa mara nyingine.

“Utofauti wetu ndio nguvu yetu na umoja wetu ndio nguvu zetu,” alisema Pelosi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles