22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Guinea wamfukuza kocha wao

CONAKRY, GUINEA

CHAMA cha soka nchini Guinean, kimethibitisha kumfukuza kocha wao Paul Put mara baada ya kuondolewa kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika nchini Misri.

Maamuzi ya kuchana na kocha huyo yamekuja mara baada ya chama hicho cha soka kukutana na Waziri mwenye dhamana ya michezo nchini humo mapema Jumatatu.

Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya pamoja na Burkina Faso raia wa nchini Ubelgiji, alichukua jukumu la kuinoa Guinea mwaka 2018 na kuifanya timu hiyo ifuzu Mataifa ya Afrika hatua ya makundi.

Katika hatua hiyo ya makundi, Guinea ilifanikiwa kushinda mchezo mmoja, kufungwa mmoja na kutoa sare mmoja, hivyo kuwafanya wafanikiwe kuingia hatua ya 16 bora kwa ‘best loser’ ila safari yao ilifikia mwisho kwenye michuano hiyo baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Algeria katika hatua ya mtoano.

Kutokana na matokeo hayo, uongozi wa timu hiyo ukafikia makubaliano na kuvunja mkataba na kocha huyo na sasa wapo kwenye mipango ya kutafuta mwingine.

“Uongozi wa timu ya taifa umefikia makubaliano ya kuchana na kocha Paul Put mara baada ya kukutana na waziri wa michezo, hivyo baada ya muda tutatangaza kocha mpya ambaye atachukua nafasi hiyo,” walisema chama cha soka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles