27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Belmadi: Siwezi kuwaahidi Algeria

CAIRO, MISRI

KOCHA wa timu ya taifa Algeria, Djamel Belmadi, amedai hana mpango wa kuwaahidi mashabiki wa timu katika mchezo wao wa fainali kesho kutwa dhidi ya Senegal.

Algeria wamefanikiwa kuingia hatua hiyo baada ya kupata bao la ushindi katika dakika ya mwisho ya mchezo dhidi ya Nigeria ambapo mchezo huo ulimalizika kwa ushindi wa mabao 2-1, mwishoni mwa wiki iliopita.

Bao la kujifunga la William Troost-Ekong pamoja na bao la mwisho la Riyad Mahrez yaliwafanya kuingia fainali huku Senegal wakiingia hatua hiyo baada ya kuwachapa Tunisia.

Belmadi mbali na kikosi chake kuonekana kuwa bora, lakini anaamini anakwenda kukutana na moja ya timu bora barani Afrika, hivyo hawezi kutoa ahadi kwa mashabiki.

“Mimi sio mchawi wala, lakini niliwaambia Algeria kuwa, nitahakikisha ninafanya kila liwezekanalo kwa ajili ya kuwafanya wawe na furaha, ila siwezi kuwaahidi suala la kutwaa ubingwa kwa kuwa haupo mikononi mwangu.

“Kitu muhimu ni kuhakikisha tunashinda mchezo huo uli kuwa mabingwa, kila mmoja kati yetu anapambana kwa ajili ya taji hilo hata wapinzani wetu akili yao ipo kwenye ubingwa wa michuano hiyo.

“Hivyo ninaamini mchezo huo utakuwa mgumu sana na tayari tumeanza kufanya maandalizi kwa ajili ya fainali hiyo,” alisema kocha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles