23.6 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Nigeria wajipa matumaini mshindi wa tatu

CAIRO, MISRI

BAADA ya timu ya taifa Nigeria kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Algeria, kiungo wa timu hiyo Moses Simon, amedai wanataka kuhamishia nguvu zao kwa wapinzani Tunisia kwa ajili ya taji la mshindi wa tatu.

Mchezo huo wa kuwania nafasi ya mshindi wa tatu unatarajiwa kupigwa leo ambapo Nigeria watashuka dimbani kupambana na Tunisia ambao walifungwa bao 1-0 dhidi ya Senegal katika mchezo wa nusu fainali.

Kupoteza kwa Nigeria katika mchezo wa nusu fainali kunaifanya timu hiyo iwe imepoteza mara ya tano kati ya sita walizofika hatua hiyo katika michuano ya Afcon.

“Tumeumizwa sana kwa kitindo cha kushindwa kuingia hatua ya fainali, nadhani hatukustahili kupoteza nafasi hiyo dhidi ya wapinzani wetu Algeria.

“Tukiwa kama wachezaji, tumejipanga kwa ajili ya mchezo wetu wa mwisho wa kumtafuta mshindi wa tatu, tunaamini nguvu zetu zote tutazihamishia huko ili kuwafanya mashabiki wawe na furaha,” alisema kiungo huyo.

Katika historia ya Tunisia kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika imefanikiwa kushinda mara moja katika ya mara tatu walizofika hatua hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,097FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles