22.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mchungaji atuhumiwa kumbaka mwanawe, walimu wawili kumpa mimba mwanafunzi

Walter Mguluchuma-Katavi

JESHI la Polisi Mkoa wa Katavi limemtia mbaroni Mchungaji Boaz Yohane (56) wa Kanisa la FPCT kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake wa miaka 17 na kumpa mimba. 

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga, alisema mchungaji huyo alikamatwa juzi saa nne asubuhi.

Alisema mchungaji huyo alikuwa akiishi na mtoto wake huyo wa kike ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Kenswa.

Kamanda Kuzaga alisema mtuhumiwa alitumia nafasi  ya kuishi na mtoto huyo kufanya naye mapenzi kwa kumlazimisha hadi kumpa ujauzito.

Alisema polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema ambao walikuwa hawapendezwi na mwenendo wa mchungaji huyo.

“Baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa, ndipo tulianza kufanya uchunguzi na kuweka mtego ambao tulifanikiwa kumnasa mchungaji ambaye hadi sasa bado tunaendelea na mahojiano naye na tukikamilisha tutamfikisha mahakamani kwa hatua za sheria,” alisema.

Katika tukio jingine, Kamanda Kuzaga alisema wanawashikilia walimu wawili wa Shule ya Msingi Kambuzi, Tarafa ya Ndurumo wilayani Mpanda  kwa tuhuma za kumbaka  kwa nyakati tofauti na kumpatia ujauzito mwanafunzi.

Alisema mwanafunzi huyo ni wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Kambuzi.

Kamanda Kuzaga aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Ambukile Mwakapala (30) na John Ndenje ambao wote wanafundisha Shule ya Msingi Kambuzi.

Alidai kuwa watuhumiwa hao walimbaka mwanafunzi huyo  kwa nyakati tofauti, na walikamatwa Julai 10, mwaka huu katika Kijiji cha Kambuzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles