Mr. T Touch: Nidhamu inapoteza wasanii

0
950

Mr T TouchNA MWANDISHI WETU

PRODYUZA wa muziki nchini, T Touch amesema wasanii wengi wanapotea kwenye muziki kwa kuwa hawana nidhamu ya muziki na wanaowazunguka.

“Wasanii wengi waliofanikiwa na kufikia malengo yao wana nidhamu kubwa kwa wanaowazunguka hasa wadau na mashabiki wa muziki, hapa nyumbani kuna vipaji vingi lakini vinapotea kwa kukosa nidhamu hasa wanapoanza kuona mafanikio.

“Wasanii wengi ninaokutana nao katika kazi yangu huwa na nidhamu wanapokuja kuomba kufanyakazi nami lakini baadhi yao wakianza kufanikiwa huwa na dharau na baada ya muda hupoteza vipaji vyao kwa kuwa hukosa msaada kila wanapokwenda,” alisema T Touch.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here