29.9 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Navy Kenzo wagombewa kimataifa

navyNA SHARIFA MMASI

PRODYUZA na msanii wa Bongo Fleva, Nahreel na Aika Mareale, wanaounda kundi la Navy Kenzo, wamesema wamepokea maombi ya idadi kubwa ya wasanii wa kimataifa wanaotaka kufanya nao kazi.

Nareal alisema kwamba, maombi hayo kutoka kwa wasanii hao ambao hakutaka kuwaweka wazi kwa kuwa bado hawajakamilisha makubaliano yao yametokana na kufanya vizuri kwa video ya wimbo wao wa ‘Game’ waliomshirikisha Vanessa Mdee.

Nahreel aliongeza kwamba, video ya wimbo huo imekuwa ikichezwa katika vituo mbalimbali vya runinga ndani na nje ya nchi ambapo imewawezesha kufanya mahojiano ya moja kwa moja na vituo vingi vya redio na televisheni na kuongeza chachu ya wasanii wengi kutaka kufanyakazi na wasanii wa kundi hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles