Baby J atua ‘Mkubwa na Wanawe’

0
1164

Baby JNA CHRISTOPHER MSEKENA

LICHA ya kuwa na kipaji msanii ni lazima uwe chini ya uongozi na usimamizi mzuri wa kazi zako ili uyafikie mafanikio, hii ameitambua msanii kutoka visiwani Zanzibar, Jamila Abdallah ‘Baby J’, mara baada ya kutangaza kuwa chini ya kituo cha Mkubwa na Wanawe.

Akizungumzia maamuzi yake hayo, Baby J, alisema kwa muda mrefu amekuwa akifanya kazi zake bila ya kuwa na uongozi kitu kilichompotezea muda na kuyachelewesha mafanikio yake licha ya kuwa na kipaji.

“Wasanii wote waliofanikiwa huwa wanakuwa na uongozi ambao unaratibu kazi zao, ni vigumu kwa msanii kufanikiwa bila kuwa na usimamizi ndiyo maana nimeamua kufanya kazi chini ya uongozi wa Mkubwa na Wanawe ili nifikie ndoto zangu kwenye muziki,” alisema Baby J.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here