26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, May 26, 2022

Lupita: Wazazi wanataka niolewe

Lupita-8NEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa filamu nchini Kenya ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani, Lupita Nyong’o, amesema wazazi wake wanamshawishi aolewe ili wapate wajukuu.

Lupita kwa sasa anafanya vizuri katika filamu nchini Marekani na amefanikiwa kuchukua tuzo za Oscar mapema mwaka huu, hivyo baada ya kupata tuzo hiyo alitembelea nchini Kenya na kukutana na familia yake ambapo ilimtaka aolewe.

“Nilipokuwa nchini Kenya wiki chache zilizopita nilikutana na familia yangu ambapo miaka mingi tulikuwa hatujakutana, lakini mama yangu aliniambia kuwa huu ni muda wa kutafuta mtoto hivyo natakiwa kuolewa.

“Lakini kila kitu kina wakati wake, ninaamini muda ukifika nitaolewa na nitapata watoto kama wazazi wangu wanavyotaka kuwa na wajukuu,” alisema Lupita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,379FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles