25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 26, 2022

Kifo cha Kristina Brown, chanzo chajulikana

KristinaATLANTA, MAREKANI

BAADA ya kifo cha mtoto wa aliyekuwa nyota wa muziki nchini Marekani, Whitney Houston, Kristina Brown, kutokea mapema Julai mwaka huu, shirika la uchunguzi wa kifo hicho, The Fulton County Medical Examiner limesema limepata majibu ya kifo hicho.

Hata hivyo, shirika hilo limesema kuwa haliwezi kuweka wazi chanzo cha kifo hicho kwa ajili ya usalama.

Awali kulikuwa na taarifa kwamba chanzo cha kifo hicho kilitokana na kuwekewa sumu kwenye kinywaji chake huku akishutumiwa mpenzi wake, Nick Goldon.

Kristina alikutwa ameanguka bafuni kwake mjini Atlanta ambapo ilikuwa Januari 31 mwaka huu na kupoteza fahamu kwa miezi sita mpaka anapoteza maisha Julai 26.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,404FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles