25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Mr Flavour ampigania Diamond Nigeria

NA CHRIS MSEKENA

STAA wa muziki pande za Nigeria, Mr Flavour, amemwagia sifa Diamond Platnumz kwa mafanikio makubwa aliyonayo licha ya vyombo vya habari nchini humo kutompa heshima anayostahili.

Katika mahojiano aliyofanya mwishoni mwa wiki na mtangazaji, Ebuka Uchendu, Mr Flavour amelalamika watangazaji na madj wa Nigeria kuupa nafasi kubwa muziki wa Afro Beat na kuziacha aina nyingine za muziki kama Bongo Fleva, Lingala, High Life nk.

“Diamond anafanya muziki mzuri hata ukiangalia YouTube ana namba kubwa kuliko wasanii wengi wa Marekani lakini hapa Nigeria hapati nafasi kwa sababu redio na TV nyingi zimejifungia kwenye boksi moja la Afro Beat ni mara ngapi umesikia wakimuongelea Diamond, mimi siwezi kubadili aina ya muziki wangu wa High Life hata kama haupewi nafasi nyumbani ila kuna nchi zinausikiliza sana,” amesema Mr Flavour ambaye alishawahi kufanya ngoma mbili na Diamond Platnumz, Nana na Time to Party zilizofanya vizuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles