27.1 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Jackson Jack, Aline Gahongayire waachia ‘Nyemerera’

Na CHRIS MSEKENA

KUTOKA nchini Marekani, mwimbaji wa Injili, Jackson Jack, amerudi kivingine na wimbo, Nyemerera, aliomshirikisha staa wa muziki huo kutoka Rwanda, Aline Gahongayire.

Jackson Jack, amesema anamshukuru Mungu kwa kukamilisha wimbo huo wa Kimataifa unaokwenda kuwaleta watu wengi kwa Mungu na kukuza huduma yake.

“Nyemerera ni wimbo wa kusifu na kumwabudu Mungu, video imeshatoka ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube ya Jackson Jack, naomba sapoti kwa mashabiki zangu hapo Tanzania na Afrika Mashariki yote pia namshukuru Aline Gahongayire kwa kushiriki kwenye baraka hii, video imefanyika hapa Marekani na Rwanda na imeongozwa na It’s Dieudonne na Bob Chris Raheem huku audio ikitengenezwa na Boris,” amesema Jackson Jack.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles