30.8 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Naslim Tz afurahia kunogesha Madina Event

Na CHRIS MSEKENA

MKALI wa muziki wa Kaswida Bongo, Naslim Haroun ‘Naslim Tz’, amesema anafurahia kupata nafasi ya kunogesha onyesho la Madina Event lililofanyika mwezi uliopita jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia tukio hilo, Naslim amesema ni ngumu kupata nafasi hiyo ni adimu ila kwa uwezo wa Allah aliweza kuimba Kaswida kadhaa ukiwemo wimbo wake maarufu, Mwambieni Dini Haichezewi.

“Onyesho kubwa la Madina Event limeniongezea wafuasi, watu wengi wameguswa na wimbo wangu Mwambieni Dini Haichezewi, natarajia kufanya mambo makubwa zaidi ili kuupaisha muziki wa Kaswida ndani na nje ya Tanzania, kwa sasa mashabiki wa Kaswida wanaweza kutembelea chaneli yangu ya YouTube (Naslim Tz) kuona kazi zangu nyingine nilizofanya na zitakazokuja,” amesema Naslim.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles