28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Mastaa Bongo wahimizwa kuvaa mavazi ya Kiafrika

NA JEREMIA ERNEST

MBUNIFU mchanga wa mavazi ya asili nchini, Aloyce Donald, amewaomba mastaa kwenye kiwanda cha burudani kutangaza utamaduni wa Afrika kwa kuvaa nguo za malighafi (material) za Kiafrika.

Mbali na ubunifu wa mavazi asili, Aloyce Donald ni mwasisi wa tamasha la African Asset, ambalo hufanyika kila mwisho wa mwaka na huambatana na utolewaji wa tuzo kwa wadau wa mitindo ili kutambua mchango wao.

Akizungumza na wandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Donald amesema wasanii wengi wameacha kutumia mavazi yanayo tangaza bara la Afrika na kuutukuza mavazi ya kigeni.

“Tasnia ya burudani inakuwa kwa kasi barani Afrika, kupitia wasanii tunaweza kutangaza rasilimali zetu pamoja na mavazi ambayo yanatokana na matirio (malighafi) zetu. Nikiwa kama mdau wa utamaduni niwaombe waweze kutumia mavazi ya kiafrika kama Kanga, Kitenge na Batiki ili kutangaza asili yetu katika mabara mengine,” amesema Aloyce Donald.

Aliongeza kuwa malighafi za Kiafrika zinaweza kutengeneza mavazi mbalimbali ambayo unaweza kuvaa kwenye mitoko yote na ukaonekana nadhifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles