24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mpoto awa Balozi mapambano ya Ukimwi

mpotoooNA BEATRICE KAIZA

MGODI wa dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya Kupambana na Kudhibiti Ukimwi nchini (Tacaids), imemteua msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto kuwa Balozi wa Kampeni ya ‘Kili Challenge’ ambaye atakuwa akielimisha jamii kuhusu mapambano ya Ukimwi.

Mpoto alisema amefurahia kuaminiwa na kupata fursa ya kipekee kwa kudai kwamba wataweza kupunguza vifo vya walioathirika na ugonjwa huo kwa kushirikiana.

“Naomba nitoe wito kwa Watanzania na Waafrika wote tuendelee na mapambano dhidi ya Ukimwi, tuzungumze na tuchukue hatua ili ugonjwa huu wa Ukimwi upungue, Tanzania bila Ukimwi inawezekana kama tutakuwa mstari wa mbele kuzidi kutoa elimu na kutumia njia sahihi za kujikinga na ugonjwa huu,” alisema Mpoto.

Mpoto aliendelea kufafanua kwamba lengo la kampeni hiyo ni  kutoa elimu juu ya ugonjwa huo vijijini na mjini.

“Hakuna kisichowezekana, tuhakikishe Tanzania  tunafikia idadi ya zero katika maambukizi mapya, zero ya  unyanyapaa na vifo vitokanavyo na Ukimwi inawezekana,” alimaliza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles