Ne-Yo kutua nchini Mei 19  

Neyo na Ali kibaNA MWANDISHI WETU

MWIMBAJI maarufu duniani wa miondoko ya R&B kutoka nchini Marekani, Ne-Yo, anatarajia kufanya ziara nchini mwezi huu kwa mwaliko wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania na Jembe Media Limited.

Ne-Yo anayetamba na wimbo wa ‘Let Me Love You’, ‘Beautiful Monster’, ‘Coming With You’ na  ‘She Knows’ aliomshirikisha Juicy J anatarajiwa kuwasili nchini Mei 19.

Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Matina Nkurlu, alisema msanii huyo akiwasili nchini atatoa burudani katika tamasha litakalofanyika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mbali na kukonga nyoyo za wapenzi wa muziki msanii huyo atashiriki katika shughuli za kusaidia jamii.

Naye mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wa Tamasha hilo, Costantine Magavilla, alisema tamasha hilo litasambaza burudani ya muziki kona zote za Tanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here