31.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 5, 2022

Contact us: [email protected]

Mourinho kumwalika Guardiola baada ya ‘Manchester Derby’

mourinho-kumwalika-guardiolaNEW YORK, MAREKANI

KOCHA wa timu ya Manchester United, Jose Mourinho, amesema ataendeleza utamaduni wa kupongezana  kwa kumwalika mpinzani wake, Kocha wa Manchester City,  Pep Guardiola,  glasi ya mvinyo ofisini kwake baada ya mchezo wao wa ‘Manchester Derby’ utakaochezwa kesho uwanja wa Old Trafford.

Kocha hao wa zamani wa Barcelona na Real Madrid, wapo katika presha  ya kufanya vizuri katika mchezo huo ambao utawakumbusha  uhasama wao wa zaidi ya miaka 20 tangu wakiwa pamoja katika kabu ya Barcelona.

Akiwa katika mkutano na waandishi wa habari jana jijini Manchester, Mourinho alisisitiza  mchezo huo hauna uhusiano  wowote  na makocha  hao badala yake utakuwa wa kuonesha uwezo kwa wachezaji wa timu hizo. Hata hivyo, wakati Guardiola akiulizwa kama angekuwa na mlo na Mourinho, kocha huyo alipendekeza  jambo hilo lingetokea bila ya wao kupanga.

Katika mkutano huo, Mourinho alionesha  kusikitishwa  na uadui uliokuwapo baina yao na kuamua kumwalika mpinzani wake baada ya mchezo huo.

Guardiola hadi sasa bado hajaamua  kukubali mwaliko huo  ambao  utamkutanisha  na kocha ambaye wamekuwa katika upinzani mkali zaidi kwa sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,586FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles