31.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 5, 2022

Contact us: [email protected]

Azam: Muda bado kufurahia ushindi

azNa Pendo Fundisha, Mbeya.

UONGOZI wa timu ya Azam FC, umesema licha ya kufanikiwa kuchukua pointi tatu muhimu na kuvunja mwiko kwa Tanzania Prisons, haiwezi kufurahia ushindi huo kutokana na mechi ngumu iliyopo mbele yao dhidi ya Mbeya City.

Msemaji wa timu ya Azam, Jaffary Iddy, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati yao na Tanzania Prisons, ambapo timu yake iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Alisema kikubwa ni kwamba bado hawana furaha licha ya kufanikiwa kuchukua pointi tatu kwa Prisons, akieleza furaha hiyo itakamilika kama watafanikiwa kuishinda timu ya Mbeya City.

“Bado tupo Mbeya tunaendelea kujiandaa na mchezo wetu unaofuata dhidi ya Mbeya City, tumekuwa na bahati ya kushinda katika mechi zetu na Mbeya City, tunataka tushinde na hii.

“Tumefanikiwa kuvunja mwiko kwa kuifunga timu ya Prisons, hiyo ni historia kwani Prisons wamekuwa wagumu kufungika katika uwanja wao wa nyumbani na wana takribani mechi 25, wamecheza bila kufungwa katika uwanja wa Sokoine,” alisema Iddy.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,586FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles