24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni ya Marekani yanunua  Formula 1

bernie-ecclestone NEW YORK, MAREKANI

KAMPUNI  ya Liberty Media ya Marekani, imethibitisha  kununua  mashindano ya mbio za  Formula 1 kwa  dola za Marekani bilioni nne.

Uamuzi wa kampuni hiyo  umedaiwa   kuvunja  minong’ono ya mwaka mmoja uliopita kuhusu mmiliki halali wa mbio hizo.

Hata hivyo, Bernie Ecclestone, atabaki kuwa  Mkurugenzi  Mkuu wa  mashindano hayo lakini Makamu Mwenyekiti wa  Kampuni ya 21 Century Fox, Chase Carey, atakuwa  Mwenyekiti mpya wa kampuni hiyo.

Kampuni ya Liberty Media inadaiwa  kuwekeza katika  michezo  na burudani mbalimbali  duniani.

Kampuni hiyo inayomilikiwa  na  bilionea, John Malone, pia ina mpango wa  kununua hisa  kutoka  kwa  kampuni nyingine  ambazo zinamiliki  mashindano makubwa ya mbio za magari duniani.

Kampuni hiyo ilinunua mashindano hayo kwa jumla ya bilioni nane kwa kujumuishwa bilioni nne za Marekani ambazo zilitolewa kwa kulipa deni  la mashindano hayo.

Liberty Media ilinunua hisa kutoka kampuni binafsi ya CVC Capital ambayo  ilikuwa ikizimiliki tangu 2012.

Lakini kampuni hiyo imekuwa ikikosolewa kwa  kuchukua faida kubwa     katika michezo, ambayo imekuwa na mdororo wa  haki ya matangazo  miaka ya hivi karibuni.

Mhariri wa uchambuzi wa michezo wa Kampuni ya BBC Sport,  Dan Roan, alisema kwamba ununuzi huo ni wa kihistoria  katika michezo ambao ulikuwa muhimu kufanyika kwa ajili ya  mashindano hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles