27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

Moto wazua taharuki NMB Mtwara

FLORENCE SANAWA, MTWARA

Jaribio la kuzima moto limezua taharuki kwa wateja na watumishi wa benki ya NMB tawi la Mtwara baada ya kuona moshi ukiwa umetanda ndani ya benki hiyo na kusababisha sintofahamu iliyopelekea watu kukimbia na kutoka nje ya jengo. 

Akizungumza na Mtanzania Digital, Pili Adolafi amesema kuwa tukio hilo liliwapa wasiwasi mkubwa kabla hawajajua kuwa ni majaribio ambapo imewasaidia kupata elimu kwa vitendo jambo ambalo litamuwezesha kuepuka majanga ya moto yanapotokea. 

“Tunaishukuru benki ya NMB  kwa kutoa elimu hii ya zimamoto kwa vitendo bila kupata haya mafunzo pengine tusingekuwa na uelewa wowote wa masuala haya naamini serikali inaweza kutusaidia ili tupate elimu ya uokoaji hasa tunapokumbwa na majanga” amesema Adolafi.

Naye Hamis Mpalala  mkazi wa Mtwara amesema kuwa zoezi hilo ni funzo kubwa kwakuwa liliandaliwa vizuri na litasaidia endapo litatokea Kweli.

Mimi nilifika benki nikaona moshi mara tukatolewa nje zimamoto wakafika lakini hili jambo lazima liangaliwe maisha tuliyonayo yamejaa magonjwa mengi ni vyema ikaangaliwa namna ya kufanya ili kunusuru maisha ya watu wenye matatizo mbalimbali” amesema Mpalala.

Meneja wa tawi hilo, Dereck Fidelis amesema kuwa wamefanya zoezi hilo kama jaribio la usalama kwa wateja na watumishi ili kuwapa elimu ya masuala ya usalama wanapopatwa na madhara ya moto. 

“Kwa mujibu wa sheria taasisi za kifedha zinapaswa kufanya majaribio ya majanga hili halikuwa tukio la moto bali lilikuwa ni tukio la kuangalia namna gani tunaweza kupata msaada haya majaribio yanatutaka kujiandaa mali zeni zote zipo salama” amesema Fidelis.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles