27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

Wasanii wapongeza juhudi za Magufuli

TUNU NASSOR 

Baadhi ya wasanii wa filamu wanawake wameridhishwa na utekelezaji  wa miradi ya maji uliofanywa serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA).

Wasanii hao wametembelea miradi ya mbalimbali ya maji leo kwa nyakati tofauti wamemshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kumtua ndoo kichwani mwanamke.

Mmoja wa wasanii hao Snura Mushi amesema katika serikali ya awamu ya tano imeboresha upatikanaji wa huduma ya maji safi hasa mkoa wa Dar es Salaam.

“Rais amepania kumtua ndoo kichwani mwanamke na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa,”amesema Snura. 

Naye Coletha Raymond amesema kazi iliyofanywa na serikali ni kubwa hivyo ni jukumu la wananchi kuunga mkono kwa kulipia ankara zao za maji.

“Tumetembelea miradi ya maji na kushuhudia kazi iliyofanywa hatuna budi kuishukuru serikali yetu,” amesema Coletha.

Kwa upande wake Halima Yahya ‘Davina’ amesema awali hali ya upatikanaji wa maji ulikuwa mgumu sasa yapo kwa asilimia kubwa.

“Tumeshuhudia mitambo mikubwa iliyowekezwa hivyo mimi binafsi naamua kuchagua mafanikio,”amesema Davina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles