27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

DC Ikungi ahamasisha wananchi kushiriki uchaguzi Serikali za Mitaa

Mwandishi Wetu

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Edward Mpogolo amewataka wananchi wa wilaya hiyo kutumia muda uliobaki kujiandikisha katika daftari la uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili waweze kutumia haki yao kuchagua viongozi.

Mpogolo amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Kitongoji cha Mtakuja, Kijiji cha Ikungi katika Wilaya hiyo alipokwenda kujiandikisha, aliwataka wananchi wa Ikungi kutumia haki yao ya Kidemokrasia ya kuchagua na kuchakuliwa.

Aidha amesema uchaguzi ngazi wa serikali ngazi ya Vitongoji na Vijiji ni muhimu wananchi hushiriki moja kwa moja kupanga na kuamua kutekeleza maendeleo yao.

“Hivyo ni muhimu kwa kila mwana Ikungi kushiriki kwakuwa inaamua hatima yake ya kujiletea maendeleo ambayo Rais John Magufuli amekuwa akipambana kwa watanzania,” amesmea.

Amesema wameshaandika kura zaidi ya asilimia 41  ambapo wameweka mikakati kuhakikisha wanafikia lengo la kuandikisha watu 154137.

Mpogolo amewahimiza wananchi aliowakuta katika kituo hicho  pamoja na vituo vingine alivyotembelea kuwahimiza vijana wao ambao umri wao ni juu ya miaka 18 kuhakikisha nao wanajiandikisha ili waweze kupata nafasi ya kuchagua viongozi ambao watawaletea maendeleo.

“Wazee wangu, tuwahimize na vijana wetu nyumbani nao wajiandikishe tusikubali wakabaki bila kujiandikisha nafasi hii ni muhimu kuitumia ili nao wawe sehemu ya kuchagua viongozi wanaowataka,” alisema Mpogolo.

Aidha, amesema maendeleo katika nchi hayawezi kushuka kutoka Mbinguni bali kwa kuchagua viongozi imara, wenye mapenzi na maendeleo ya wananchi na pia maendeleo ya nchi yao.

Mpogolo alitembelea vituo vingine katika wilaya hiyo ambapo alizungumza na wananchi kujua changamoto zao katika uandikishaji huo na pia kuwahamasisha kuwashauri na watu wengine kujitokeza.

“Msiwaache watu nyumbani tuhakikishe wote wanajiandikisha, kina mama nyumbani, majirani,” alisema.

Aidha amesema katika wilaya hiyo uandikishaji unaenda vizuri, watu wanajitahidi kujitokeza na pia viongozi wanajitahidi kuhamasisha wananchi kujitokeza ili kuhakikisha kila mmoja anashiriki kupiga kura.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles