25.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 6, 2024

Contact us: [email protected]

MNEC Simiyu awaasa viongozi wakuchaguliwa kutatua kero za wananchi

Na Mnwandishi Wetu, Meatu

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (MNEC) Mkoa wa Simiyu, Emmanuel Gungu amewataka Viongozi wa kuchaguliwa na Wananchi kutatua kero za Wananchi wao sio kuwa watu wa kulalamikia Serikali ya awamu ya sita.

MNEC Gungu ametoa kauli hiyo leo Janauari 28, 2024 wilayani Meatu wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki mbili alizozitoa kwa kwa askari wa Wanyamapori katika Pori la Akiba Maswa kwenye Jimbo la Kisesa ili kusaidia kuongeza nguvu ya kuwadhibiti Wanyama hao wakali.

Amesema viongozi wa kuchaguliwa na wananchi wanajua jinsi serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan inavyoleta maendeleo kwa wananchi.

Gungu aliwataka Viongozi wa kuchaguliwa na Wananchi, waache kuilalamikia Serikali na kuisema kila kukicha, kwani wao kazi yao nikuhakikisha wanawasikiliza wananchi na kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.

“Ndugu Jeremiah Shilingi Katibu wa Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amewasilisha maombi kwamba watu wanacheleweshwa kulipwa fidia, kwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa.

“Naomba nikwambie ukamwambie mheshimiwa mbunge suala hilo lipo mikononi mwake, kwani mbunge ndiye anayetunga sheria, kusimamia sheria na kuwaelimisha wananchi, hivyo yeye atusaidie kwakuwa wao ndio wanaotunga sheria hizo,” alissema Gungu na kuongeza:

“Hata Diwani wetu wahapa Tindabuligi unanafasi ya kutusaidia huko kwenye Serikali, kumaliza changamoto za wananchi siyo mnalalamika tu jamani mtusaidie muwasaidie wananchi. Diwani unaingia huko kwenye vikao vya Halmashauri unauwezo wa kupigania mambo ya maendeleo ya wananchi na yakafanyika,” amesema Gungu.

Gungu amesisitiza kwamba lazima viongozi wamsaidie mheshimiwa rais kutatua changamoto za wananchi ambazo zipo ndani ya uwezo wao na kwamba sio kila kitu lazima afanye Mheshimiwa Rais wakati wasaidizi wake wapo.

“Jamani siyo kila kitu lazima afanye Mheshimiwa Rais wakati sisi wasaidizi wake tupo, mengine tufanye sisi wenyewe tumsaidie, kwani yeye ana mambo mengi yakufanya, hivyo tunayoweza kufanya tufanye sisi,” amesema Gungu.

Awali, Diwani wa Kata ya Tindabuligi, Tabu Maghembe akiwasilisha taarifa yake alisema anamshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha Sh bilioni 1.8 kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Kata ya Tindabuligi.

Mjumbe huyo ametoa Pikipiki hizo mara baada ya kupokea, maombi ya kuwasaidia Wananchi katika Jimbo hilo ambao bado wanasumbuliwa na Tembo na kuhalibiwa mali, chakula na makazi yao.

Akizungumzia pikipiki hizo, Afisa Mhifadhi wa Pori la Akiba Maswa, Lawrence Okode amemshukuru Mjumbe Gungu kwa kusaidi kununua Pikipiki mbili ambazo alieleza zitakuwa msaada mkubwa kupunguza usumbufu wa Wananchi kushambuliwa na tembo.

“Kwanza, kwa niaba yangu naomba nikushukuru sana. Nilitaka kuanza kuzitumia hizi pikipiki, lakini kutokana na mvua ungeikuta imechakaa, niliamua kusubiri uje utukabidhi na leo umekuja nakusukuru sana Mheshimiwa Mnec,” amesema Okode.

Mapema, kupitia mkutano uliyowakutanisha Makatibu Kata, Madiwani na Wananchi wa Jimbo la Kisesa Mnec huyo pia ameahidi kuzungumza na wadau wengine ili kusaidia kupatikana kwa Pikipiki nyingine zisizopungua 10.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles