24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 8, 2024

Contact us: [email protected]

Mmoja akamatwa na meno ya tembo Tunduru

Na AMON MTEGA-SONGEA

JESHI la Polisi Wilaya ya Tunduru, Mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na maofisa wa wanyamapori wilayani humo, wamefanikiwa kukamata meno mawili ya tembo ambayo thamani yake haijafahamika.

Akizungumza ofisini kwake jana, Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Ruvuma, Pili Mande, alisema tukio hilo lilitokea  Februari 2, mwaka huu, majira ya saa sita usiku katika Kijiji cha Semeni kilichopo wilayani humo.

Alifafanua kuwa askari polisi pamoja na maofisa wa Idara ya Wanyamapori (KDU) kwa pamoja walipokuwa katika doria, walimkamata Issa Bony (44), mkazi wa Kijiji cha Semeni akiwa na meno mawili ya tembo.

Kaimu Kamanda Mande alisema jeshi hilo linaendelea na upelelezi wa kujua mtuhumiwa aliyapata wapi meno hayo na alikuwa akiyapeleka wapi.

“Pia, tunataka kujua ni silaha gani iliyotumika kumuulia mnyama huyo na ili kukomesha uwindaji haramu ambao umekuwa ukifanyika kwenye maeneo mbalimbali ikiwamo kwenye Wilaya ya Tunduru na Namtumbo kutokana na kuwepo kwa Pori la Hifadhi la Akiba la Selous, hatua zinazostahili zitachukuliwa dhidi ya mtuhumiwa huyo ili liwe fundisho kwa wengine.

“Wilaya ya Tunduru ipo jirani na Hifadhi ya Pori la Akiba la  Selous  na inapitiwa na sehemu za mapitio ya wanyama.

“Mapitio hayo ya wanyama ambayo ni maarufu kama ushoroba, yamepita kwenye maeneo ya vijiji vya wilaya hiyo na kuelekea nchi jirani ya Msumbiji kupitia Bonde la Mto Ruvuma.

“Pamoja na jiografia hiyo, hatuwezi kuruhusu watu waue wanyama pori bila sababu ndiyo maana tunalazimika kufanya doria za mara kwa mara ili kukabiliana na wahalifu,” alisema Kaimu Kamanda Mande.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles