27.6 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Mbaroni kwa kumbaka mtoto wa miaka 16

NAVELINE KITOMARY NA MARRY NYARI 

-DAR ES SALAAM 

MKAZI wa Tegeta Machinjioni, Dar es Salaam, Shadrack Myaule (24), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa shtaka la ubakaji. 

Akisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Joyce Mushi, karani wa mahakama hiyo, Matarasa Hamisi, alidai Desemba 16 na 23 mwaka jana, mshtakiwa alimbaka mtoto mwenye miaka 16 katika eneo la Tegeta Machinjioni, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na Hakimu Mushi alisema kuwa dhamana yake iko wazi na atatakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaotoa bondi ya Sh.milioni 1.

Mshtakiwa alirudishwa rumande kwa kushindwa kukidhi masharti ya dhamana hadi kesi yake itakaposomwa tena Februari 18, mwaka huu.

Wakati huo huo, watu watatu wamepandishwa  kizimbani kwa shtaka la kupiga na kujeruhi.

Waliopandishwa kizimbani ni Nicksoni Miti (34), Flora James (39) na Salome Sangali (16) wote wakazi wa Mabibo.

Wakisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Hanifa Mwingira, Mwendesha mashtaka wa Jamhuri, Credo Rugaju alidai kuwa Julai 7 mwaka jana katika eneo la Mabibo washtakiwa walimpiga Mary Laus kwa kutumia ndoo ya plastiki na kumsababishia majeraha mbalimbali katika mwili wake. 

Washtakiwa walikana kutenda kosa hilo na Hakimu Mwingira alisema kuwa dhamana yao iko wazi na kila mshtakiwa atatakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaotoa bondi ya Sh milioni 1.

Washtakiwa walirudishwa rumande kwa kushindwa kukidhi masharti ya dhamana hadi kesi yao itakaposomwa Februari 18, mwaka huu.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,186FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles